Kiswahili

Nduguföreningen inaleta mabadiliko!


Ni NGO yenye makao makuu nchi ni Sweden, malengo yake ni kusaidia katika kazi za kuleta maendeleo ama mabadiliko ya maisha katika Tanzania. Mkoa wa Singida, wilaya ya Iramba, tarafa ya Kinamapanda , kata ya Ulemo, kijiji cha Misigiri na mtaa wa Kizaga.


Kwa kushirikiana na wanajamiii wa Kata ya Ulemo. Nduguföreningen tumeweza kutenda kazi  nyingi katika maeneo haya;

Elimu, afya, mazingira, kuwapatia wanajamii mikopo isiyo na riba, maji safi na salama.


Twashirikiana kwa karibu mno na serikali; Halmashauri ya Iramba  magharibi, wanakijiji, na wadau wengine wanaopenda kuleta maisha bora katika jamii.


Msingi wetu katika kazi zote ni kupeleka mambo yote karibu na walengwa na kuwashirkisha walengwa katika kila jambo. Twaamini kwamba, maendeleo yataletwa na  wanajamii wenyewe. Nduguföreningen inawawezesha katika utekelezaji wa majukumu.


Kanuni nyingine katika kazi zote ni ahadi za muda mrefu.


Chama chetu hakifungamani na upande wowote(ki siasa wala Kidini)


Chama hiki kilianzishwa 2002. Tangu wakati huo kimeendelea kujitangaza na kupata wanachama wengi zaidi mwaka kwa mwaka. Katika kipindi hiki kifupi tumewawezesha  wanafunzi  zaidi ya 200 kupata Elimu katika shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na vyuo vikuu. Tumeweza kupanda miti  zaidi ya elfu 10, kwa kuzuia uharibifu wa mazingira na momonyoko wa Udongo, chama kimechangia katika mradi wa maji safi kijijini Misigiri, upande wa afya  kimesaidiana na serikali katika ujenzi wa Zahanati ya kijijji , nyumba za watumishi , umeme wa mionzi ya jua  na samani( vifaa), kuendelesha  semina za UKIMWI katika shule na viongozi wa vijijii vya kata na mitaa. Tumeendesha semina za kilimo, mikopo midogo na biashara na mazingira.


Mafanikio yote yametokana na ushirikiano mwema kati yetu ,serikali na wanajami i wa  Iramba.


Kwa michango ya wanachama wa Ndugu walioko duniani kote , wanatusiaidia  kuleta matumaini, kujiamini na kuwa na uwezo wa kutoa watu katika maisha duni. Shukurani  kwa michango ya hali na mali kwa wote.


Kwa  yeyote anayependa kutoa michango yake ya hali na mali,  twakukaribisheni sana!


Barua pepe yetu ni  ordforande@ndugu.org